TEKNOLOJIA INAVYOWEZA KUFANYA MAKUBWA

Font size:

Shalom!

Leo nimeandaa taarifa ya kazi mbalimbali, ambazo zimefanywa na wanateknolojia sehemu tofauti tofauti duniani kama moja ya jitihada za kutumia kipaji cha ubunifu walichojaliwa na Mungu.

Nikianzia nchini Marekani, ambapo Mwanzilishi wa Amazon, ambayo ni biashara kubwa duniani ya mauzo ya bidhaa mtandaoni, Jeff Bezos amepanga kupeleka mwezini chombo cha anga za mbali.

Bezos anayemiliki shirika la utafiti wa anga na urubani lijulikanalo kama Blue Origin, amesema wamepanga kurusha mwezini chombo cha shirika hilo chenye uwezo wa kubeba roboti nne za utafiti. 

Chombo hicho kipya kina ukubwa unaolingana na chumba chenye umbo la wastani kwa maana ya si kikubwa sana au kidogo sana na kitarushwa kwenda mwezini kwa kutumia roketi mpya yenye nguvu kubwa na injini zilizobuniwa kisasa.

Bezos ambaye pia ni mmiliki wa jarida la Washington Post, alitambulisha mfano wa chombo hicho ambacho kitarushwa kuelekea mwezini katika ofisi za shirika la Blue Origin hivi karibuni.

Inaelezwa kuwa Bezos hakufahamisha ni lini haswa chombo hicho kitafanya safari hiyo ya kwenda mwezini, wala hakusema kama chombo hicho kitabeba watu.

Makamu wa Rais wa Blue Origin, Clay Mowry, amesema wanatarajia ifikapo mwaka 2024 safari za binadamu kuelekea mwezini zitafanyika mara kwa mara.

Naye mshauri maalumu wa masuala ya anga wa shirika hilo, Robert Walker, amesema wamepanga kufanya safari zisizojumuisha watu kwenda mwezini kabla ya kutamatika kwa mwaka huu.

ITAENDELEA...

Mwandaaji ni William Shechambo,

0687 05 28 93.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook