MKURUGENZI MAWASILIANO IKULU, MAWAZIRI WATETA NA WANAHABARI IKULU DAR ES SALAAM

Font size:

Mkurugenzi wa wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, akiambatana na mawaziri na watendaji waandamizi wa taasisi kadhaa za serikali, amekutana na wanahabari, Ikulu ya Dar es Salaam, leo Nov. 15, 2023.

Zuhura amesema Rais Samia akiwa nchini Morroco, alishiriki kwenye jukwaa la uwekezaji ambapo aliinadi Tanzania kimataifa kwa ajili ya mataifa hayo kuja kuwekeza nchini Tanzania.
                                                        
Amesema, Rais pia alishiriki kwenye ufunguzi na majadiliano katika jukwaa la uwekezaji la mwaka 2023 kuhusu kuharakisha mageuzi ya kiuchumi barani Afrika na uwasilishwaji wa miradi ya kimkakati iliyopo kwenye nchi husika. 

"Sekta zilizopewa kipaumbele kwenye miradi ya kimkakati ni viwanda, madini, nishati, usafirishaji pamoja na utunzaji wa mazingira," amesema.

Pia amewaeleza wanahabari kuwa, Rais alieleza washiriki wa jukwaa hilo, umuhimu wa kujenga mradi wa reli ya kisasa kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay, lengo likiwa ni kupata fedha za kuendeleza mradi huo.

Kadhalika, amesema akiwa Saudi Arabia, Rais alishiriki kwenye mkutano wa Taasisi ya Mfuko wa maendeleo ya Saudi Arabia ambapo Saudi Arabia imewekeza dola za Marekani mil. 533 ili kuendeleza mataifa ya Afrika na Tanzania. 

"Rais Samia alishuhudia utiaji wa saini hati za makubaliano kati ya Tanzania na Saudi Arabia kwenye soko la ajira la wafanyakazi na wafanyakazi wa ndani, makubaliano ya Tanzania kupatiwa mkopo wa shilingi bil. 32 katika sekta ya nishati kwenye mradi wa umeme wa Benako Kyaka," amesema.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook