Font size:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 17, 2023 amempokea Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wawili, wamepata nafasi ya kuteta faragha na kujadili masuala kadhaa ya kudumisha mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Rais huyo atakuwepo nchini kikazi hadi Novemba, 19 mwaka huu.