ASKOFU NASSARI AIMWAGIA SIFA MAKUMIRA SEKONDARI IKITIMIZA MIAKA 50

Font size:

Askofu KKKT, Dayosisi ya Meru, Elias Kitoi Nassari, ameupongeza uongozi wa Shule ya sekondari ya Makumira kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.


Amesema mafanikio hayo yanatokana na jitihada za walimu na wanafunzi pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule na wazazi, walezi wanaopeleka wanafunzi shuleni hapo.

Pongezi hizo amezitoa wakati akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 50, tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikiwa na KKKT, Dayosisi ya Meru.

Askofu Nassari amesema, umri wa shule hiyo, unatosha kabisa kuwa mtaji mzuri wa kuongoza harakati za mabadiliko chanya katika sekta elimu.

Aidha amewataka wanafunzi wa shule za Kanisa, kuzingatia masomo yao shuleni na kuwa mabalozi wazuri katika jamii, ili wawe chachu ya maendeleo ya Taifa.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook