DKT. MALASUSA ASISITIZA MWENDELEZO KANISA KUWASAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

Font size:

Mkuu wa KKKT Mteule, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dkt. Alex Gehaz Malasusa, amesema Kanisa litaendelea kuwasaidia Watoto wenye Mahitaji Maalumu bila kujali Itikadi za Kiimani, huku akisisitiza Watanzania wote kupendana kama Mungu anavyowapenda.

Askofu Dkt. Malasusa amesema hayo leo, Nov. 17, 2023, wakati akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Shule ya Mtoni Maalumu, yaliyofanyika katika Kituo hicho cha Kanisa Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Serikali, ambapo amesema kupitia elimu walioipata Watoto hao, anaamini jamii itabadilika na kuacha kuwanyanyapaa Watoto wengine wa namna hiyo.

Dkt. Malasusa ameagiza idara inayohusika na Idara ya Udiakonia Dayosisi, pamoja na Bodi ya Udiakonia kutangaza rasmi tarehe ya kufungua Chuo Cha Mlandizi VTC, Ili Watoto waliopatiwa Elimu ya awali Mtoni Maalumu waendelee na Mafunzo katika chuo hicho.

Msaidizi wa Askofu Dean Chediel Lwiza, pamoja na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu Watoto hao Kwa niaba ya Askofu Dkt. Malasusa, amesema ili Watoto hao wajifunze, wanahitaji muda mrefu hivyo ameiomba Serikali, Taasisi, Wazazi, Walezi na Walimu kushirikiana ili kuwasaidia pamoja na wazazi ambao Watoto wao wamehitimu kuwa Mabalozi wazuri kwa wengine.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Udiakonia DMP, Jane Kamugisha, ameomba Serikali kushughulikia kusaini makubaliano ya Uendeshaji wa Kituo hicho na Serikali huku Mratibu wa Kituo, Winfrida Malumbo, akisema bado kuna idadi kubwa ya Watoto wanaohitaji kupatiwa Mafunzo lakini Kituo hicho kinapokea Watoto 100 tu kutokana na Miundombinu iliyopo.

Mmoja wa Watumishi waliotoa huduma kituoni hapo kwa muda wa zaidi ya miaka 30, Rebeka Beke, amesema ukilinganisha na awali, Kanisa lilipoanzisha kutoa huduma hizo watu wengi hawakuwa na uelewa kwamba Watoto wenye Ulemavu wa akili wanaweza kujifunza.

Mratibu wa Chuo cha Mlandizi VTC, Caroline Shedaffa, amesema chuo hicho kitafunguliwa mapema mwakani na kwamba wanatarajia kutangaza tarehe rasmi hivi karibuni.

✍🏾 Vincent Kasambala

#Upendomedia #Amanikwawote

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook