Je unafahamu nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya makanisa, karibu kwenye makala hii fupi tukujuze zaidi...
1. Vatican
Kwa upande wa idadi ya watu, nchi ya Vatican haiwezi kufikia idadi ya watu hata ya nchi moja barani Ulaya. Ikiwa ungependa kuona nchi iliyo na makanisa mengi, nafasi yako nzuri zaidi ni kwenda moja kwa moja hadi Jiji la Vaticani. Ina makanisa mengi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.
Vatican ina takriban makanisa 1,700 na kuifanya kuwa nchi yenye makanisa mengi, Idadi hiyo imezidi idadi ya wakazi ambao ni 1000 pekee.
2. Marekani
Nchi ya Marekani ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na Wakristo wengi lakini nchi hiyo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na makanisa mengi duniani ikiwa na jumla ya makanisa 360,000.
3. Brazil
Brazili, taifa kubwa zaidi bara la Amerika Kusini, ina idadi kubwa ya makanisa ambayo ni ya Kiprotestanti na Kanisa Katoliki. Kuna takriban makanisa 190,000 katika taifa hilo ambalo Ukristo ulianza wakati wa utawala wa kikoloni wa Ureno.
4. Russia
Russia ni miongoni mwa nchi zenye orodha ya makanisa mengi duniani ambapo inatajwa kuwa katika nchi hiyo kuna makanisa 150,000, Kanisa la
Orthodox Russia ndiyo linaongoza kwa idadi kubwa ya makanisa.
Kwa mujibu wa christiangist.com, wastani wa kila jengo moja la Kanisa linaweza kuchukua wananchi wa Urusi 975 na ifahamike kuwa jumla ya
wananchi wa Russia ni zaidi ya milioni 146.
5. China
Nchi ya China licha ya changamoto nyingi kwa wakristo bado idadi ya majengo ya kuabudia kwa wakristo ni mengi ambapo inaelezwa kuwa jumla ya makanisa 130,000, yanapatikana ndani ya Jamhuri ya Watu wa China. Inaelezwa kuwa Kanisa moja linaweza kuchukua watu 11,032 na Idadi ya wananchi wa China ni zaidi ya Bilioni 1.5.
6. Nigeria
Kwa upande wa Afrika nchi ya Nigeria ndiyo kinara wa idadi kubwa ya makanisa ambapo inelezwa kuwa nchi hiyo yenye wakazi Milioni 206, ina
makanisa 100,000 yanayotambulika na serikali nchini humo.
Hivi karibuni mji wa Lagos, ulitajwa kuwa ndiyo kinara kwa idadi ya makanisa Afrika, na mji huo unapatikana Nigeria. Kila Kanisa moja
nchini Nigeria linaweza kutumiwa kuabudu na watu 2,066.
7. Italia
Italia inatajwa kama kitovu cha Kanisa Katoliki, lakini ndani ya nchi hiyo inapatikana Vatican, Italia ukiitoa Vatican inatajwa kuwa na
makanisa 50,000 huku asilimia 80 ya wakazi wa Italia wakiwa ni wakristo kati ya watu Milioni 60.
8. Ujerumani
Ujerumani imebeba historia kuu ya Matengenezo ya Makanisa na Ukristo katika nchi hii ni sehemu ya historia na utamduni, Ujerumani inatajwa
kuwa na makanisa 45,000 huku makadiro kwa kila jengo la Ibada ikiwa na uwezo wa kutumia kuabudu na watu 1,861.
9. Poland na Malawi
Nchi hizo mbili moja ikiwa inapatikana barani Ulaya (Poland) na nyingine Afrika zote kwa pamoja zina makanisa zaidi ya 10000 kwa upande wa Poland wakristo wengi ni kutoka waprotestanti.
10. Spain, Rwanda, Angola na Romania
Nchi hizo zinatajwa kwenye orodha ya nchi zenye makanisa mengi kutokana na takwimu kuonesha kuna makanisa ya zaidi ya 2,000 katika
nchi hizo ambayo yanaendana na wastani wa wakristo waliopo nchini hizo. Ikiwa na maana kuwa kila Kanisa linaweza kuchukua angalau watu 300 ili kila Kanisa liwe na waumini.
MAKALA HII NI KWA MSAADA NA CHRISTIANGIST.COM, BSCHOLARLY.COM RNN.NG