Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Upendo Media Network, Nengida Johannes, akiambatana na Mkuu wa Maudhui ya Upendo FM Radio, Upendo Tuheri, wamekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso na Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo.
Mazungumzo ya pande hizo mbili yamefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya MultiChoice Tanzania, zilizopo jijini Dar es Salaam.
Upendo TV, inayomilikiwa na Upendo Media Network, ni miongoni mwa chaneli makini duniani zenye maudhui ya dini, ambazo zinarushwa na kisimbuzi cha DSTV, ambacho kwa ukanda huu kinasambazwa na kusimamiwa na MultiChoice Tanzania.
Ungana nasi UPENDO TV kupitia chaneli namba 388, DSTV.
#Upendomedia #Amanikwawote