Font size:
Dayosisi ya Ziwa Tanganyika ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imekamilisha mchakato wa kumpata mrithi wa Askofu Ambele Mwaipopo, aliyemaliza muda wake kwa kumchagua Mchungaji Imani Kibona, katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika uchaguzi huo, Mchungaji Zebedayo Mbilinyi aliyekuwa Mkuu wa Jimbo la Katavi katika Dayosisi hiyo, amechaguliwa kuwa Msaidizi wa Askofu Mteule.
Taarifa za kuaminika ambazo Upendo Media imezipata kutoka Makao Makuu ya Dayosisi hiyo, zinasema Askofu Mteule Kibona ambaye alikuwa Msaidizi wa Askofu Mwaipopo, anatarajiwa kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini, Aprili, mwaka huu.