NI AFCON YA AINA YAKE

Font size:

Katika hali isiyotarajiwa, mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Senegal, usiku wa kuamkia leo Januari 30, 2024 wametupwa nje ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast na wenyeji ambao ni timu ya taifa hilo.

Ivory Coast iliishinda Senegal 5-4 kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi yao ya jana na kufuzu kwa hatua ya robo fainali. Timu hizo mbili zilikuwa zimetoka sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo wao wa hatua ya 16 bora, ambao pia uliongezewa muda kikanuni.

Habib Diallo anayeitumikia klabu ya ligi kuu ya Saudi ya Al-Shabab, alikuwa ameifungia Senegal bao la kwanza dakika ya 4, lakini Ivory Coast ilijikomboa kwa kuchelewa na kufunga bao la kusawazisha dakika ya 86 kupitia kwa mkwaju wa penalti wa Franck Kessie.

Kufuatia matokeo hayo, Ivory Coast itacheza dhidi ya Mali au Burkina Faso katika robo fainali, wikiendi hii, siku ya Jumamosi.

Senegal ilishinda taji la AFCON msimu uliopita, kwa kuichapa Misri 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 0-0 katika fainali ya michuano hiyo iliyoandaliwa na Cameroon mwaka 2021.

Hadi sasa, Ivory Coast wameshinda mikwaju yao 11 ya penalti katika Kombe la Mataifa ya Afrika, zaidi ya timu nyingine yoyote katika mashindano hayo. Wameshinda mechi tano kati ya hizi 11 za mikwaju ya penalti, huku Misri pekee ikiwa na idadi kubwa ya mabao 6.

Ivory Coast wametinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya 11 katika historia yao, huku awamu hii wakiwa na matokeo hafifu zaidi tangu kuanza kwa kampeni hiyo, baada ya kupenya 16 bora kwa kushinda mechi moja tu katika kundi lao (best looser).

Hili ni mara ya saba mfululizo, ambapo bingwa mtetezi ameshindwa kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook