LOWASSA AFARIKI DUNIA

Font size:

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.

Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

"Lowassa amefariki akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu. Hayati Ngoiyai Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14 mwezi Januari mwaka 2022," Alisema Dkt. Mpango

Alikuwa akipatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya moyo kisha kupelekwa Afrika Kusini na baadaye kurudishwa tena katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook