Waimbaji nyimbo za injili, kwaya mikopo hadi milioni 100

Font size:

Waimbaji wa nyimbo za Injili, vikundi vya kwaya na wadau mbalimbali wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kupitia sekta ya utamaduni na sanaa ili kujiinua katika kazi zao.

Akizungumza leo Septemba 19, 2023 kwenye kipindi cha Hali Halisi  cha 107.7Mhz Upendo FM , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Nyakaho Mahemba amesema mfuko huo umeanzishwa na Serikali kwa ajili ya kuwainua wasanii, wadau mbalimbali wa sanaa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kusaidia ununuzi wa vifaa vya kuzalishia kazi za wasanii hao na fedha za uendeleshaji wa uzalishaji.


Amesema  Serikali inatambaua kwamba changomoto ya wasanii hao ni mitaji hivyo wanashindwa kuzalisha kazi bora kutokana na ukosefu wa mitaji ambapo baadhi ya changamoto inayowakumba wasanii ikiwemo kuanzisha, kukuza, elimu na kuendeleza kazi hizo, serikali hiyo baada ya kubaini hilo inatoa mkopo wa masharti nafuu kwa mtu mmoja mmoja, vikundi na makampuni ili waweze kuzalisha kazi bora zitazokidhi soko la ndai na nje.

"Serikali imeanzisha mikopo ya masharti nafuu na kiwango cha chini cha mkopo huo ni Shilingi 100,000 na cha juu Shilingi milioni 100 na riba yetu ni nafuu sana ambayo asilimia 9 inayotozwa katika salio la mkopo. Tunamshukuru Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuiheshimisha sekta hii na dhamila yake ni kuzalisha ajira nyingi katika nchi yetu kupitia sekta hii kwa kutambua kwamba vijana wengi wanaangukia katika sekta hii’’. Amesema

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook