Font size:
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamiaji (IOM) limesema kuongezeka kwa ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kumefanya idadi ya wa wakimbizi wa ndani kufikia milioni 6.9.
Shirika hilo limesema Kongo inakabiliwa na mojawapo ya mgogoro mkubwa zaidi wa kibinaadamu duniani na kwamba kufikia Oktoba 23, takriban watu milioni 5.6 ambao ni wakimbizi wa ndani, walikuwa wakiishi katika majimbo ya mashariki ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Ituri na Tanganyika.
IOM imesema watu hao wanahitaji pakubwa misaada ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Mgogoro kati ya waasi wa M23 na wanamgambo watiifu kwa serikali ya DRC umeongezeka katika jimbo la mashariki la Kivu Kaskazini tangu mapema mwezi huu hasa kaskazini mwa Goma.