Font size:
Diwani wa Kikristo aliyesimamishwa uanachama wake wa Conservative baada ya kuonesha msimamo wake wa kidini juu ya wapenzi wa jinsia moja amerejeshwa kazini huku akiweka msisitizo kuwa hatoweza kupinga msimamo wake kwa kuwa Ukristo unapinga vitendo hivyo na kila mwamini anajua.
King Lawal, ambaye amekuwa diwani ndani ya Halmashauri ya Northamptonshire kwa miaka miwili, aliondolewa uanachama mwaka huu, baada ya kuchapisha kwenye mtandao wa X (zamani ikijulikana kama Twitter) kwamba mapenzi ya jinsia moja ni ushirika wa kishetani na ukristo haukubali ushetani huo ndani ya Kanisa.
Punde baada ya kuchapisha maneno hayo aliondolewa katika nafasi za kiungozi katika mashrika aliyokuwa ana ushirikiano nayo kisha alilazimishwa kujiuzulu kutoka kwa kampuni yake mwenyewe, ambayo alikuwa ameijenga na kuikuza.
Akiungwa mkono na Kituo cha Kisheria cha Kikristo (CLC), Bw Lawal alikuwa akijiandaa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya chama chake akidai kuwa ni ukiukwaji wa haki zake za uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuabudu". Hata hivyo, mapema wiki hii Diwani huyo alirejeshwa kazini kufuatia uchunguzi wa Kamati ya Maadili ya mamlaka ya eneo hilo.
Kufuatia uamuzi huo, Mhe. Lawal alionyesha kufarijika kwake na anatumai kwamba Ofisi Kuu ya Chama cha Conservative, ambayo bado inachunguza kesi kuhusu uanachama wake, itafikia hitimisho sawa na Kamati ya Maadili ya Halmashauri Northamptonshire.
Lawal aliwahimiza watu "kusimamia kile wanachoamini" na kutosita kuongea ukweli juu ya Ukristo dhidi ya vitendo vyote vya kinyume na mapenzi ya Mungu kwa kuongea Imani ya Ukristo sio chuki.