HUYU NDIYE ELON MUSK

Font size:

Elon Reeve Musk, kama ambavyo amepewa majina haya na familia yake, alizaliwa Juni 28 mwaka 1971 mjini Pretoria, Transvaal, nchini Afrika Kusini, na sasa ana uraia wa nchi tatu, ambazo ni Marekani, Afrika Kusini na Canada.

Huyu ni mmoja kati ya wawekezaji wakubwa duniani kwenye sekta ya teknolojia, akiwa na utajiri wa takriban dola milioni 19.2 (sawa na sh. trilioni 44.1 za kitanzania) na anatajwa kuwa mmoja kati ya wajasiriamali wengi wenye maono hai katika dunia ya leo.

Jambo maalumu kuhusu Elon Musk ni hamu yake ya kutokwama licha ya hatari ambazo wengine wanaziona kwenye uwekezaji hasa wa kiteknolojia hivyo kuwafanya kurudi nyuma na kutafuta sekta nyingine ya kuwekeza.

Kitaaluma ni Mhandisi na wakati huu akiwa na miaka 52 tu, tayari Musk anahusika na kampuni kadhaa zenye uwekezaji wa mabilioni ya dola ikiwa ni pamoja na PayPal, Tesla Motors, SolarCity, Zip2, SpaceX, Open ambayo sasa ina mradi mkubwa wa Hyperloop unaohusika na utengenezaji wa treni ya kasi zaidi inayotumia nishati ya umeme na mtandao wa X ambao awali ulifahamika kwa jina la Twitter.

Oktoba mwaka 2002, kutokana na mafanikio ya kampuni yake ya kwanza ya PayPal, wawekezaji wengi walivutiwa nayo na kupanda dau wakitaka kuinunua kwa fedha nyingi tu lakini kampuni ya mauzo ya mtandaoni inayofahamika kwa jina la ebay, ilishinda zabuni na kuinunua PayPal kwa dola za kimarekani bilioni 1.5.

Elon kama nilivyoeleza awali, ana moyo wa uthubutu, bila woga, aliamua kutoa fedha alizokuwa nazo kama akiba, na kuwekeza kwenye mambo makubwa na kabambe, katika sayansi na teknolojia ikiwemo ya magari ya michezo (Tesla) na yale yanayotumia nishati ya umeme, treni pamoja na sayansi ya anga.

Maono ya Elon Musk ni kuanzisha mji katika Sayari ya Mirihi (Mars), ambayo ni sayari ya nne katika mfumo wetu wa jua.

Anasema ana lengo la kutuma kundi la pili la watalii kwenye sayari hiyo kufikia mwaka 2024 lakini gharama ya safari hiyo tiketi itakuwa dola bilioni 10.

Mtu wa kwanza kunufaika na fursa hiyo ni Dennis Tito (82), ambaye ni mhandisi mstaafu aliyetumia siku nane mwaka 2001, katika kituo inachojulikana kwa jina la ISS.

Elon alipoulizwa na waandishi mbalimbali wa masuala ya teknolojia, alisema lengo la kuja na wazo la safari hizo ni kupunguza hatari ya kupotea binadamu kwa kufanya ubinadamu kuwa huru kwa aina mbalimbali za sayari na ustaarabu wa ulimwengu wa anga.

Kauli hii ilihusianishwa na hofu aliyokuwa nayo na kuitangaza hadharani kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Teknolojia ya Massachussetts (MIT) mwaka 2014, kuwa anahofia teknolojia ya akili bandia yaani Artificial Intelligence, itaua kizazi cha binadamu duniani.

Alinukuliwa akisema uvumbuzi kwenye teknolojia ni pumzi kwa maendeleo ya teknolojia duniani, lakini kwenye suala la AI, ana hofu kuwa binadamu hawajafikiria juu ya kesho yao dhidi ya ufumbuzi huo unaoonekana kuwa na dalili za kutawala dunia miaka michache ijayo.

Kwa Elon kuja na wazo la kuanzia mji Mars, watu wengi walidhani alikuwa mwendawazimu lakini yeye aliwapinga kwa vitendo kwa kuamua kuwekeza fedha nyingi kwenye kampuni ya Space X inayohusika na kutimiza ndoto hiyo.

Mwanzo haukuwa rahisi, yeye pamoja na kikosi chake cha wataalamu waligonga mwamba mara kadhaa kwenye majaribio yao ya ubunifu wa roketi ya kwenda Mirihi na aliyumba kiuchumi kiasi cha kukopa fedha kwa marafiki zake ili kujaribu kukuza biashara yake.

Walijaribu tena roketi yao ya Spaceships ya uzinduzi ulikuwa ni janga hivyo Musk na timu yake waliamua kufanya jaribio la moja la mwisho ambapo kwa mujibu wa Musk, kama jaribio la hilo la nne wangelishindwa, kampuni yake ingekuwa bila rasilimali ya kuendeleza biashara na angefilisika kabisa.

Anasema lakini kwa kujiamini kwake, uzinduzi huo wa nne wa roketi ulikuwa wa mafanikio, na mambo yakageuka kua mazuri kiasi cha NASA, kumuita na kikosi chake kisha kutangaza kwamba kampuni yake, SpaceX, imekuwa mshindi wa dola bilioni 1.5 na kuwapa mkataba wa kufanya kazi na NASA.

Hakika mafanikio ya Elon Musk kama mjasiriamali, mwekezaji na mhandisi ni ya kipekee, kupitia yeye teknolojia inaendelea kukua kwa kasi lakini somo hapa ni kuwa ana moyo wa kujiamini, kujaribu na bila kukata tamaa.

Muandaaji ni William Shechambo, kwa msaada wa Intaneti.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook