POLISI DRC YASAMBARATISHA MAANDAMANO

Font size:

Jeshi la Polisi nchini DRC, limelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya maandamano yaliyoitishwa na upinzani katika mji mkuu wa Kinshasa, wakitaka kurudiwa kwa uchaguzi wa Rais na wabunge uliofanyika wiki iliyopita na kuzua taharuki.


Uchaguzi huo unaodaiwa kuwa na utata mwingi, unatishia kuliyumbisha taifa hilo ambalo tayari linakabiliana na tatizo la usalama upande wa mashariki, hali inayotajwa na wachambuzi wa kisiasa Afrika kudumaza maendeleo huku likiongoza duniani kwa uzalishaji wa madini ya cobalt na mengine muhimu.


Wagombea watano wa urais, ambao ni wapinzani wakuu wa Rais Felix Tshisekedi kwenye uchaguzi huo waliwaomba wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano ya leo Jumatano mchana, ili kupinga zoezi la uhesabuji kura hivyo libatilishwe.


Waliapa kuendelea na maandamano hayo hata baada ya serikali kuyapiga marufuku Jumanne kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya DRC, Peter Kazadi, ikisema kwamba yanahujumu kazi ya tume ya taifa ya uchaguzi, CENI, wakati ikiendelea na zoezi la kukusanya matokeo, ambapo kwa sasa yanaonyesha kuwa Rais Tshisekedi anaongoza kwa kura nyingi.


Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, polisi walizingira makao makuu ya mgombea mmoja wa upinzani, Martin Fayulu, ambako waandamanaji walitarajiwa kukusanyika tangu majira ya Asubuhi.


or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook