WATHEOLOJIA 17 WABARIKIWA KUWA WACHUNGAJI KONDE

Font size:

Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Konde Geoffrey Mwakihaba, amewataka Wachungaji wa Kanisa hilo kuwa na hofu ya Mungu katika kuifanya kazi yao na kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Hayo amesemwa wakati akiongoza Ibada Maalumu ya kuwabariki na kuwaingiza kazini Wachungaji 17 wa Dayosisi hiyo, Ibada iliyofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Tukuyu na kuwataka Wachungaji hao kutumika vizuri shambani mwa Bwana.

Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Konde, Benjamini Mbembela, akisoma hati ya kuwabariki Wachungaji hao, alisema Askofu anawajibu wakuwabariki Wachungaji kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo.

Baadhi ya Wachungaji walioingizwa kazini akwemo Tusajigwe Katefu na Lusajo Solomon, wakizungumza katika Ibada hiyo walisema, watakuwa waaminifu katika nafasi zao ikiwemo kutuza viapo vyao vya Uchungaji.

Naye Katibu Mkuu wa Jimbo la Tukuyu, Wille Ngailo na Mwinjilisti wa Usharika huo Ezra Mbenanga, waliwapongeaza Wachungaji hao kwa kubarikiwa kwani wanakwenda kutumika shambani mwa Bwana.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook