WANANCHI SENGEREMA WAPEWA ELIMU YA FEDHA, MIKOPO

Font size:

Wananchi wametakiwa kukopa mikopo inayotolewa na Serikali na taasisi rasmi, ili kujiepusha na udhalilishaji unaoweza kutokea kutokana na kukopa mikopo yenye masharti magumu kutoka kwa taasisi zisizo rasmi na kwa wakopeshaji binafsi.

 

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Binuru Shekidele, alipokutana na jopo la wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake na kueleza kuwa mikopo rasmi hufuata taratibu za kisheria ambazo zinalinda haki za wakopaji.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Jacob Nkungu, amewashauri watoa huduma za fedha kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi bila kuwakandamiza.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook