Font size:
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, amesema Tanzania
inaendelea na dhamira yake ya kushiriki katika kutekeleza Ajenda ya
Maendeleo ya Afrika 2063, kupitia uwekezaji wa kimkakati katika sekta
mbalimbali kama vile miundombinu ya usafirishaji, nishati, kilimo, viwanda,
TEHAMA, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya rasilimali watu.
Dkt. Mpango amesema hayo alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika
Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Bodi ya Juu ya Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA - NEPAD), uliyofanyika kwa njia ya Mtandao
na kuongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye ni Rais wa Misri Abdel Al Fattah
El - Sisi.
Kadhalika Makamu wa Rais amesema, ni muhimu nchi za Afrika kuimarisha vyanzo
vya mapato vya ndani, kwa kutumia vyema rasilimali za nchi kama vile madini
pamoja na kushirikiana na sekta binafsi ili kukabiliana na upungufu wa fedha za
ufadhili wa miradi katika kutekeleza Ajenda 2063.