Font size:
Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, ameongoza Ibada maalumu ya kuweka wakfu gari jipya la Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Ibada hiyo imeambatana na tukio la kukata utepe gari hilo, kama ishara ya chombo hicho cha usafiri kuanza kazi rasmi, tukio lililofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya KKKT yaliyopo jijini Arusha, leo Feb. 28, 2025.