ASKOFU MALASUSA ATOA RAI UJENZI WA KITOPENI

Font size:

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex Gehaz Malasusa, ametoa wito kwa Wakristo na Watanzania wote wenye mapenzi mema, kushiriki kuchangia Ujenzi wa kituo kipya cha kulelea na kufundishia watoto wenye mahitaji maalumu cha Udiakonia Kitopeni, kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kitopeni, wilayani Bagamoyo.


Dkt. Malasusa ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, amesema wakristo wanawajibu wa kuwasaidia wahitaji kwa upendo wa Mungu bila kujali  rangi, dini ama kabila na kuhamasisha kila mmoja kushirikimwa uwezo wake baraka za ujenzi wa kituo hicho unaotarajiwa kuanza mwaka huu.


Kadhalika, amesema hatua ya ujenzi wa kituo hicho imekuja mara baada ya kituo cha Mtoni Diakonia ambacho kipo hivi sasa kutokidhi mahitaji ya ongezeko la Watoto hao lakini pia mazingira kutokuwa rafiki kutokana na maendeleo na mabadiliko ya kidunia.


Kituo hicho kitakapokamilika kitakuwa cha kwanza katika Afrika na nchi hii.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook